Ronaldinho kumpeleka Coutinho Barcelona ?
Nyota wa zamani wa Barcelona Ronaldinho Gaucho amesema anatamani sana kumuona Philippe Coutinho anahamia Barcelona na kuvaa jezi ambayo yeye amevaa.
Philippe Coutinho amekuwa akiwindwa na Barcelona tangu mchezaji mwingine kutoka Brazil Neymar atimkie Ufaransa kwenye klabu ya PSG.
"Napenda sana kuona mchezaji mwenye kipaji kama cha Coutinho anavaa jezi niliyovaa mimi kwa miaka mingi”, amesema Ronaldinho kwenye mahojiano na Sky Sports, kuelekea mchezo wa leo wa kirafiki kati ya England na Brazil.
Ronaldinho ameongeza kuwa aina ya uchezaji ya Coutinho inaendana na soka la Barcelona hivyo itakuwa rahisi yeye kucheza na kupata mafanikio akiwa na klabu hiyo.
"Ninaamini jinsi anavyocheza ataendana na Barcelona ndani ya muda mfupi na atakuwa na furaha”, ameongeza Ronaldinho.
Ronaldinho alicheza Barcelona kwa misimu mitano ambapo alisajiliwa kutoka PSG mwaka 2003 na kucheza klabuni hapo hadi 2008.
No comments